21 Ikiwa mahali ambapo Yehova Mungu wenu atachagua kuweka jina lake+ ni mbali kutoka kwenu, basi mnapaswa kuwachinja baadhi ya ng’ombe wenu au kondoo wenu ambao Yehova amewapa, kama nilivyowaamuru, nanyi mnapaswa kuwala ndani ya majiji yenu wakati wowote mnapotamani nyama.