18 Siku hiyo Yehova alifanya agano+ pamoja na Abramu, akisema: “Nitaupa uzao wako* nchi hii,+ kuanzia mto wa Misri mpaka kwenye ule mto mkubwa, mto Efrati:+
31 “Nitaweka mpaka wenu kuanzia Bahari Nyekundu mpaka bahari ya Wafilisti na kuanzia nyikani mpaka kwenye Mto Efrati;+ kwa maana nitawatia wakaaji wa nchi hiyo mikononi mwenu, nanyi mtawafukuza kutoka mbele yenu.+
24 Kila mahali mtakapokanyaga kwa mguu wenu patakuwa penu.+ Mpaka wenu utaanzia nyikani mpaka Lebanoni, kuanzia ule Mto, mto Efrati, mpaka bahari ya magharibi.*+