11 Kisha Shekemu akamwambia baba ya Dina na ndugu zake: “Naomba nipate kibali machoni penu, nami nitawapa chochote mtakachoniomba. 12 Mnaweza kudai nitoe kiasi kikubwa sana cha mahari na zawadi.+ Niko tayari kuwapa chochote mtakachoniambia. Nipeni tu msichana huyu awe mke wangu.”