25 Basi Waisraeli wakachukua majiji hayo yote, wakaanza kuishi katika majiji yote ya Waamori,+ huko Heshboni na miji yake yote. 26 Kwa maana Heshboni lilikuwa jiji la Sihoni, mfalme wa Waamori ambaye alikuwa amepigana na mfalme wa Moabu na kuchukua nchi yake yote mpaka Arnoni.