-
Waamuzi 7:24, 25Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
24 Gideoni akatuma wajumbe katika eneo lote lenye milima la Efraimu, akisema, “Shukeni mkawashambulie Wamidiani, wazuieni wasivuke vijito vyote vya maji kufikia Beth-bara na pia Yordani.” Basi watu wote wa Efraimu wakakusanyika pamoja, nao wakawazuia kuvuka vijito vyote vya maji kufikia Beth-bara na Yordani. 25 Pia wakawakamata wale wakuu wawili wa Midiani, yaani, Orebu na Zeebu; wakamuua Orebu juu ya mwamba wa Orebu+ na kumuua Zeebu kwenye shinikizo la divai la Zeebu. Wakaendelea kuwafuatia Wamidiani,+ nao wakamletea Gideoni kichwa cha Orebu na cha Zeebu katika eneo la Yordani.
-