5 Akawaambia watu wa Sukothi, “Tafadhali wapeni mikate watu walio pamoja nami, kwa kuwa wamechoka nami ninawafuatia Zeba na Zalmuna, wafalme wa Midiani.” 6 Lakini wakuu wa Sukothi wakamwambia, “Je, tayari umewakamata Zeba na Zalmuna ili tuwape wanajeshi wako mikate?”