-
Waamuzi 15:4, 5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 Basi Samsoni akaenda na kuwakamata mbweha 300. Kisha akachukua mienge, akawafunga mikia wawili-wawili na kuweka mwenge mmoja kati ya kila mikia miwili. 5 Halafu akaiwasha moto ile mienge na kuwaachilia mbweha hao waingie katika mashamba ya nafaka ya Wafilisti. Basi akateketeza kila kitu kuanzia masuke mpaka nafaka iliyo shambani, na pia mashamba ya mizabibu na ya mizeituni.
-