Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwanzo 17:9, 10
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 9 Mungu akaendelea kumwambia Abrahamu: “Wewe nawe, unapaswa kushika agano langu, wewe na uzao wako* baada yako katika vizazi vyao vyote. 10 Hili ndilo agano langu nililofanya pamoja nawe, ambalo wewe na uzao wako* baada yako mtalishika: Kila mwanamume miongoni mwenu ni lazima atahiriwe.+

  • Waamuzi 14:3
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 3 Lakini baba yake na mama yake wakamwambia, “Je, huwezi kupata mke kati ya watu wetu wa ukoo na kati ya ndugu zetu wote?+ Je, ni lazima uoe mke kutoka kati ya Wafilisti wasiotahiriwa?” Lakini Samsoni akamwambia baba yake, “Niletee mwanamke huyo, kwa sababu ndiye anayenifaa.”*

  • Waamuzi 15:18
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 18 Kisha akahisi kiu sana, akamlilia Yehova akisema, “Ni wewe uliyemtumia mtumishi wako kuleta ukombozi huu mkubwa. Je, sasa nife kwa kiu na kuchukuliwa na watu wasiotahiriwa?”

  • 1 Samweli 17:36
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 36 Mimi mtumishi wako nilimuua simba na dubu pia, na huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wao, kwa sababu amevitukana* vikosi vya Mungu aliye hai.”+

  • 1 Mambo ya Nyakati 10:4
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 4 Ndipo Sauli akamwambia mtu aliyembebea silaha: “Chomoa upanga wako unichome nao, ili watu hawa wasiotahiriwa wasije kunitendea kikatili.”*+ Lakini mtu aliyembebea silaha hakutaka kufanya hivyo, kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akachukua upanga na kuuangukia.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki