17 Ndipo Yese akamwambia Daudi mwana wake: “Tafadhali, chukua hii efa ya nafaka iliyokaangwa na mikate hii kumi, uwapelekee haraka ndugu zako kambini. 18 Nawe umpelekee mkuu wa elfu mafungu haya kumi ya jibini; pia, angalia ndugu zako wanaendeleaje na uniletee kitu fulani kutoka kwao.”