15 Siku hiyo Wabenjamini walikusanya wanaume 26,000 wenye mapanga kutoka katika majiji yao, na pia wanaume 700 mashujaa kutoka Gibea. 16 Jeshi hilo lilikuwa na wanaume 700 mashujaa waliotumia mkono wa kushoto. Kila mmoja wao aliweza kurusha jiwe kwa kombeo na kulenga unywele bila kukosea.