9 Na roho mbaya kutoka kwa Yehova ikamjia Sauli+ alipokuwa ameketi nyumbani mwake akiwa na mkuki mkononi, huku Daudi akipiga muziki kwa kinubi.+ 10 Sauli akajaribu kumpigilia Daudi ukutani kwa mkuki, lakini akamkwepa Sauli, na mkuki huo ukapenya ukutani. Daudi akakimbia na kutoroka usiku huo.