22Basi Daudi akaondoka huko+ na kukimbilia katika pango la Adulamu.+ Ndugu zake na nyumba yote ya baba yake waliposikia habari hiyo, wakashuka na kumfuata huko.
5 Baada ya muda nabii Gadi+ akamwambia Daudi: “Usikae ndani ya ngome. Ondoka humo uende katika nchi ya Yuda.”+ Kwa hiyo Daudi akaondoka na kwenda katika msitu wa Herethi.
8 Wafilisti waliposikia kwamba Daudi alikuwa ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Waisraeli wote,+ Wafilisti wote wakapanda kuja kumtafuta Daudi.+ Daudi aliposikia jambo hilo, akaenda kukabiliana nao.