7 Daudi akamwambia: “Usiogope, kwa maana hakika nitakutendea kwa upendo mshikamanifu+ kwa ajili ya Yonathani baba yako, nami nitakurudishia ardhi yote ya Sauli babu yako, nawe utakula chakula* mezani pangu sikuzote.”+
28 Kwa maana wewe bwana wangu mfalme ungeiangamiza nyumba yote ya baba yangu, lakini uliniruhusu mimi mtumishi wako niwe miongoni mwa wale wanaokula mezani pako.+ Basi nina haki gani ya kuendelea kumlilia mfalme?”