-
Waamuzi 9:50-53Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
50 Kisha Abimeleki akaenda Thebesi; akalishambulia jiji la Thebesi na kuliteka. 51 Kulikuwa na mnara imara katikati ya jiji hilo, wanaume na wanawake wote, na viongozi wote wa jiji hilo wakakimbilia humo. Wakajifungia ndani yake na kupanda juu ya paa lake. 52 Abimeleki akaenda kwenye mnara huo na kuushambulia. Akaenda kwenye mlango wa mnara ili auchome moto. 53 Ndipo mwanamke fulani akaangusha jiwe la kusagia juu ya kichwa cha Abimeleki na kumpasua kichwa.+
-