-
1 Mambo ya Nyakati 20:2, 3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
2 Kisha Daudi akachukua taji lililokuwa kwenye kichwa cha Malkamu, akapata kwamba uzito wa taji hilo ulikuwa talanta moja* ya dhahabu, nalo lilikuwa na mawe yenye thamani; Daudi akavishwa taji hilo kichwani. Alichukua pia nyara nyingi sana kutoka katika jiji hilo.+ 3 Akawatoa nje watu waliokuwa ndani yake, akawapa kazi+ ya kukata mawe kwa misumeno na kufanya kazi kwa vifaa vya chuma vyenye ncha kali na kwa mashoka. Hivyo ndivyo Daudi alivyofanya katika majiji yote ya Waamoni. Hatimaye Daudi na wanajeshi wote wakarudi Yerusalemu.
-