19 Ndipo mfalme akamwambia Itai+ Mgathi: “Kwa nini wewe pia uende pamoja nasi? Rudi ukaishi na mfalme mpya, kwa sababu wewe ni mgeni, na pia ulifukuzwa kutoka katika nchi yako.
21 Lakini Itai akamwambia mfalme: “Kwa hakika kama Yehova anavyoishi na kwa hakika kama bwana wangu mfalme anavyoishi, mahali popote utakapokuwa wewe bwana wangu mfalme, ukiwa hai au ukiwa umekufa, mimi mtumishi wako nitakuwa mahali hapo!”+