36 Wana wao wawili, Ahimaazi+ mwana wa Sadoki na Yonathani+ mwana wa Abiathari wako huko pamoja nao, nanyi mtawatumia wana hao kuniletea habari zote mtakazosikia.”
17 Yonathani+ na Ahimaazi+ walikuwa wakikaa En-rogeli;+ basi kijakazi fulani akaenda na kuwaambia, nao wakaenda kumwambia Mfalme Daudi kwa maana hawakutaka kujihatarisha kwa kuonekana wakiingia jijini.