-
2 Mambo ya Nyakati 9:17-19Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
17 Mfalme pia alitengeneza kiti kikubwa cha ufalme cha pembe za tembo na kukifunika kwa dhahabu safi.+ 18 Kiti hicho cha ufalme kilikuwa na ngazi sita, nacho kiliunganishwa na kiti cha miguu cha dhahabu, na kilikuwa pia na mikono pande zote mbili, na simba wawili+ walisimama kando ya mikono hiyo. 19 Na kulikuwa na simba 12+ waliosimama kwenye ngazi hizo sita, wawili kwenye kila ngazi, mmoja upande huu na mwingine upande wa pili. Hakuna ufalme mwingine wowote uliokuwa umetengeneza kiti kama hicho.
-