19 Alikuwa akimwambia baba yake: “Kichwa changu kinauma, jamani kichwa changu kinauma!” Ndipo baba yake akamwambia mtumishi: “Mbebe umpeleke kwa mama yake.” 20 Basi akambeba na kumrudisha kwa mama yake, naye akakaa kwenye mapaja ya mama yake mpaka adhuhuri, kisha akafa.+