8 Petro akamuuliza: “Niambie, je, ninyi wawili mliuza shamba kwa kiasi hiki?” Akajibu: “Ndiyo, kwa kiasi hicho.” 9 Kwa hiyo Petro akamwambia: “Kwa nini ninyi wawili mlikubaliana kuijaribu roho ya Yehova? Tazama! Miguu ya wale waliomzika mume wako, ipo mlangoni, nao watakubeba na kukutoa nje.”