-
Mambo ya Walawi 25:4-6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 Lakini katika mwaka wa saba nchi itakuwa na pumziko kamili la sabato, sabato ya Yehova. Hampaswi kupanda mbegu wala kupunguza matawi ya mizabibu yenu. 5 Hampaswi kuvuna nafaka yoyote inayoota yenyewe baada ya mavuno, nanyi hampaswi kuchuma zabibu kutoka kwenye mizabibu yenu ambayo haijapunguzwa matawi. Ni lazima nchi iwe na mwaka wa pumziko kamili. 6 Hata hivyo, mnaweza kula mazao yanayoota nchini mwaka huo wa sabato, yaani, mtayala ninyi wenyewe, na pia watumwa wenu wa kike na wa kiume, vibarua wenu, wageni wanaoishi nanyi,
-