-
Yeremia 40:7-9Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
7 Baadaye wakuu wote wa majeshi waliokuwa uwanjani pamoja na watu wao wakasikia kwamba mfalme wa Babiloni amemweka Gedalia mwana wa Ahikamu awe msimamizi wa nchi na kwamba alikuwa amemweka awe msimamizi wa wanaume, wanawake, na watoto, watu maskini nchini ambao hawakuwa wamepelekwa uhamishoni Babiloni.+ 8 Basi wakaenda kwa Gedalia huko Mispa.+ Wakuu hao ni Ishmaeli+ mwana wa Nethania, Yohanani+ na Yonathani wana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi, wana wa Efai Mnetofa, na Yezania+ mwana wa Mmaakathi, pamoja na wanajeshi wao. 9 Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani akawaapia wao pamoja na wanajeshi wao, akisema: “Msiogope kuwatumikia Wakaldayo. Kaeni katika nchi hii na kumtumikia mfalme wa Babiloni, na mambo yatawaendea vema.+
-