5 Na mambo mengine katika historia ya Yehoyakimu, mambo yote aliyotenda, je, hayajaandikwa katika kitabu cha historia ya nyakati za wafalme wa Yuda?+ 6 Kisha Yehoyakimu akafa na kuzikwa pamoja na mababu zake;+ na Yehoyakini mwanawe akawa mfalme baada yake.