15 Alijenga kuta za ndani za nyumba hiyo kwa mbao za mierezi. Alifunika kuta za ndani kwa mbao, kuanzia sakafu ya nyumba mpaka kwenye maboriti ya dari, akaifunika sakafu yake kwa mbao za miberoshi.+
22 Aliifunika nyumba yote kwa dhahabu mpaka nyumba yote ilipokamilika; pia aliifunika kwa dhahabu madhabahu yote+ iliyokuwa karibu na chumba cha ndani zaidi.