17 Baada ya kifo cha Yehoyada, wakuu wa Yuda walikuja na kumwinamia mfalme, na mfalme akawasikiliza. 18 Waliiacha nyumba ya Yehova Mungu wa mababu zao na kuanza kuabudu miti mitakatifu na sanamu, hivi kwamba hasira ya Mungu ikaja dhidi ya Yuda na Yerusalemu kwa sababu ya hatia yao.