-
2 Mambo ya Nyakati 35:7, 8Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
7 Yosia akawachangia watu wote waliokuwepo makundi ya kondoo na mbuzi, wanakondoo dume na wanambuzi dume, kwa ajili ya dhabihu za Pasaka, jumla ya wanakondoo na wanambuzi 30,000, na pia ng’ombe 3,000. Wanyama hao walitolewa katika mali za mfalme mwenyewe.+ 8 Wakuu wake pia walitoa mchango uwe toleo la hiari kwa ajili ya watu, makuhani, na Walawi. Hilkia,+ Zekaria, na Yehieli, viongozi wa nyumba ya Mungu wa kweli, waliwapa makuhani wanyama 2,600 wa dhabihu za Pasaka na ng’ombe 300.
-