-
Ezra 4:6-8Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
6 Mwanzoni mwa utawala wa Ahasuero, waliandika mashtaka dhidi ya wakaaji wa Yuda na Yerusalemu. 7 Na katika siku za utawala wa Mfalme Artashasta wa Uajemi, Bishlamu, Mithredathi, Tabeeli, na wenzake walimwandikia Mfalme Artashasta; wakaitafsiri barua hiyo katika Kiaramu,+ na kuiandika kwa herufi za Kiaramu.*
8 * Rehumu ofisa mkuu wa serikali na mwandishi Shimshai, walimwandikia Mfalme Artashasta barua ifuatayo dhidi ya Yerusalemu:
-