2 Amka, Ee kinanda; nawe pia, Ee kinubi.+
Nitayaamsha mapambazuko.
3 Nitakusifu miongoni mwa mataifa, Ee Yehova,
Nami nitakuimbia sifa miongoni mwa mataifa.
4 Kwa maana upendo wako mshikamanifu ni mkubwa, uko juu kama mbingu,+
Na uaminifu wako, unafika mpaka angani.
5 Ukwezwe juu ya mbingu, Ee Mungu;
Utukufu wako na uwe juu ya dunia yote.+