-
Yoshua 3:15, 16Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
15 Mara tu makuhani waliobeba lile Sanduku walipofika Yordani na kutumbukiza miguu yao ukingoni mwa mto huo (kwa maana maji ya Yordani hufurika kwenye kingo zake+ sikuzote za mavuno), 16 maji yanayotoka upande wa juu yakaacha kutiririka. Yakasimama tuli kama bwawa* mbali sana huko Adamu, jiji lililo karibu na Sarethani, na yale yanayoshuka kwenye Bahari ya Araba, yaani, Bahari ya Chumvi, yakakauka. Yalisimamishwa, na watu wakavuka kuelekea Yeriko.
-