-
2 Samweli 19:34, 35Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
34 Lakini Barzilai akamwambia mfalme: “Ni siku ngapi* zilizobaki za maisha yangu hivi kwamba niende nawe mfalme mpaka Yerusalemu? 35 Leo nina umri wa miaka 80.+ Je, ninaweza kutofautisha kati ya jema na baya? Je, mimi mtumishi wako ninaweza kuonja ladha ya kile ninachokula na kile ninachokunywa? Je, bado ninaweza kusikia sauti za waimbaji wa kiume na wa kike?+ Basi kwa nini mimi mtumishi wako nikuongezee mzigo bwana wangu mfalme?
-