-
Esta 1:10-12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 Siku ya saba, moyo wa mfalme ulipokuwa umechangamka kwa sababu ya divai, akawaambia Mehumani, Biztha, Harbona,+ Bigtha, Abagtha, Zethari, na Karkasi, maofisa saba wa makao ya mfalme waliokuwa wahudumu wake binafsi, 11 wamlete Malkia Vashti mbele ya mfalme akiwa na taji la* malkia, ili awaonyeshe watu na wakuu urembo wake, kwa maana alikuwa mrembo sana. 12 Lakini Malkia Vashti akaendelea kukataa kuja, hakutii agizo la mfalme alilopewa na maofisa wa makao ya mfalme. Basi mfalme akakasirika sana, na ghadhabu yake ikawaka.
-