23 Abigaili alipomwona Daudi, alishuka haraka kutoka juu ya punda na kuanguka kifudifudi mbele ya Daudi, huku akiinama chini. 24 Kisha akaanguka miguuni pake na kusema: “Bwana wangu, acha nibebe lawama; niruhusu mimi kijakazi wako nizungumze nawe, na usikilize maneno ya kijakazi wako.