10 Nabali akawajibu hivi watumishi wa Daudi: “Daudi ni nani, na mwana wa Yese ni nani? Siku hizi watumishi wengi wanawatoroka mabwana zao.+ 11 Ninawezaje kuchukua mikate yangu na maji yangu na nyama niliyowachinjia wakataji manyoya wangu na kuwapa watu ambao hata hawajulikani wanatoka wapi?”