-
Mwanzo 46:5-7Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Kisha Yakobo akaondoka Beer-sheba, na wanawe* wakamsafirisha Yakobo baba yao na watoto wao na wake zao katika magari ya kukokotwa ambayo Farao alikuwa amewapa ili yamsafirishe. 6 Wakachukua mifugo yao na mali zao, walizokuwa wamekusanya katika nchi ya Kanaani. Basi wakafika Misri, Yakobo na wazao wake wote. 7 Alienda Misri pamoja na wanawe na mabinti zake na wajukuu wake wa kiume na wa kike—wazao wake wote.
-