-
Isaya 66:7, 8Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
7 Kabla hajawa na uchungu wa kuzaa, alizaa.+
Kabla ya kushikwa na uchungu wa kuzaa, alijifungua mtoto wa kiume.
8 Ni nani amewahi kusikia jambo kama hilo?
Ni nani ameona mambo kama hayo?
Je, nchi itazaliwa katika siku moja?
Au, je, taifa lote litazaliwa mara moja?
Hata hivyo, mara tu Sayuni aliposhikwa na uchungu wa kuzaa, aliwazaa wanawe.
-