26 Lakini Yerusalemu la juu liko huru, nalo ni mama yetu.
27 Kwa maana imeandikwa: “Furahi, wewe mwanamke tasa usiyezaa; piga vigelegele vya shangwe, wewe mwanamke usiye na uchungu wa kuzaa; kwa maana watoto wa mwanamke aliye ukiwa ni wengi kuliko wa yule aliye na mume.”+