8 Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Yehova baada ya Mfalme Sedekia kufanya agano pamoja na watu wote waliokuwa Yerusalemu ili kuwatangazia uhuru,+ 9 kwamba kila mtu awaachilie huru watumwa wake Waebrania, wa kiume na wa kike, ili mtu yeyote asimfanye Myahudi mwenzake kuwa mtumwa.