-
2 Wafalme 17:25, 26Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
25 Walipoanza kuishi humo, hawakumwogopa* Yehova. Kwa hiyo Yehova akawatuma simba waje miongoni mwao,+ nao wakawaua baadhi ya watu. 26 Mfalme wa Ashuru akapata habari hii: “Mataifa uliyoyapeleka uhamishoni na kuyaweka katika majiji ya Samaria ili yaishi humo hayajui dini* ya Mungu wa nchi hiyo. Kwa hiyo anaendelea kuwatuma simba miongoni mwao; na simba hao wanawaua, kwa sababu hakuna yeyote kati yao anayejua dini ya Mungu wa nchi hiyo.”
-