37 Lakini Eliakimu mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba,* Shebna aliyekuwa mwandishi, na Yoa mwana wa Asafu aliyekuwa akifanya kazi ya kuweka kumbukumbu wakaja kwa Hezekia mavazi yao yakiwa yameraruliwa, wakamwambia maneno ya Rabshake.
2 Kisha akamtuma Eliakimu, aliyekuwa msimamizi wa nyumba,* Shebna aliyekuwa mwandishi, na wazee miongoni mwa makuhani, wakiwa wamevaa nguo za magunia, waende kwa nabii Isaya,+ mwana wa Amozi.