26 Ndipo Eliakimu mwana wa Hilkia, na Shebna+ na Yoa wakamwambia Rabshake:+ “Tafadhali, zungumza nasi watumishi wako kwa lugha ya Kiaramu,*+ kwa maana tunaweza kuielewa; usizungumze nasi kwa lugha ya Wayahudi huku watu walio ukutani wakisikia.”+
37 Lakini Eliakimu mwana wa Hilkia, aliyekuwa msimamizi wa nyumba,* Shebna aliyekuwa mwandishi, na Yoa mwana wa Asafu aliyekuwa akifanya kazi ya kuweka kumbukumbu wakaja kwa Hezekia mavazi yao yakiwa yameraruliwa, wakamwambia maneno ya Rabshake.