8 Ataviangamiza kwa upanga vijiji vyako vilivyo mashambani, naye atajenga ukuta wa kuzingira na kujenga dhidi yako boma la kuzingira na kuinua ngao kubwa dhidi yako. 9 Ataponda kuta zako kwa mtambo wake wa kubomolea, na kubomoa minara yako kwa mashoka yake.