Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Wafalme 18:19-25
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 19 Basi Rabshake akawaambia: “Tafadhali, mwambieni hivi Hezekia: ‘Mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, anauliza, “Ujasiri wako unategemea msingi gani?+ 20 Unasema, ‘Nina mbinu na nguvu za kupigana vita,’ lakini hayo ni maneno matupu. Unamtumaini nani, hivi kwamba unathubutu kuniasi mimi?+ 21 Tazama! Unautumaini msaada wa utete huu uliopondeka, Misri,+ ambao mtu yeyote akiuegemea utamchoma kiganja na kukitoboa. Hivyo ndivyo Farao mfalme wa Misri alivyo kwa wote wanaomtumaini. 22 Nawe ukiniambia, ‘Tunamtumaini Yehova Mungu wetu,’+ je, si yeye ndiye ambaye mahali pake pa juu na madhabahu zake zimeondolewa na Hezekia,+ huku akiwaambia watu wa Yuda na Yerusalemu, ‘Mnapaswa kuinama mbele ya madhabahu hii hapa Yerusalemu’?”’+ 23 Basi sasa, tafadhali, fanya mkataba huu pamoja na bwana wangu mfalme wa Ashuru: nitakupa farasi 2,000 ikiwa unaweza kupata wapanda farasi wa kutosha idadi hiyo.+ 24 Basi, unawezaje kumzuia hata gavana mmoja aliye mdogo zaidi kati ya watumishi wa bwana wangu, huku ukiitumaini nchi ya Misri ili upate magari ya vita na wapanda farasi? 25 Sasa je, nimepanda kuja kushambulia mahali hapa ili kupaharibu bila kupewa idhini na Yehova? Yehova mwenyewe aliniambia, ‘Panda uende kuishambulia nchi hii na kuiharibu.’”

  • 2 Wafalme 19:10
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 10 “Mwambieni hivi Mfalme Hezekia wa Yuda: ‘Usikubali Mungu wako unayemtumaini akudanganye akisema: “Yerusalemu halitatiwa mikononi mwa mfalme wa Ashuru.”+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki