13 Yohanani mwana wa Karea na wakuu wote wa jeshi waliokuwa uwanjani wakaja kwa Gedalia huko Mispa. 14 Wakamwambia: “Je, hujui kwamba Baalisi mfalme wa Waamoni,+ amemtuma Ishmaeli mwana wa Nethania akuue?”+ Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu hakuwaamini.