-
Yeremia 36:22-24Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
22 Mfalme alikuwa ameketi katika nyumba ya majira ya baridi kali, katika mwezi wa tisa,* huku jiko la makaa likiwaka mbele yake. 23 Kila mara Yehudi aliposoma safu tatu au nne, mfalme aliikata sehemu hiyo kwa kisu cha mwandishi na kuitupa ndani ya moto katika jiko la makaa, mpaka kitabu chote cha kukunjwa kilipoteketea katika jiko hilo. 24 Nao hawakushikwa na hofu yoyote; wala mfalme wala watumishi wake wote waliosikia maneno hayo hawakuyararua mavazi yao.
-