25 Na Yeremia+ akamwimbia Yosia wimbo wa maombolezo, na tangu siku hiyo waimbaji wote wa kiume na wa kike+ wanaendelea kuimba kumhusu Yosia katika nyimbo zao za huzuni; na uamuzi ukafanywa kwamba nyimbo hizo zinapaswa kuimbwa katika nchi ya Israeli, nazo zimeandikwa katika nyimbo za huzuni.