66 Uhai wenu utakabili hatari kubwa, nanyi mtaogopa usiku na mchana; nanyi hamtakuwa na uhakika wa kuokoka. 67 Asubuhi mtasema, ‘Laiti ingekuwa jioni!’ na jioni mtasema, ‘Laiti ingekuwa asubuhi!’ kwa sababu ya woga mtakaohisi mioyoni mwenu na kwa sababu ya mambo ambayo macho yenu yataona.