14 Kwa maana yeye huacha mayai yake ardhini,
Na kuyapasha joto mavumbini.
15 Yeye husahau kwamba mguu fulani unaweza kuyavunja
Au kwamba mnyama wa mwituni anaweza kuyakanyaga.
16 Huwatendea wanawe kwa ukatili, kana kwamba si wake;+
Haogopi kwamba huenda kazi yake ngumu ikawa ya bure.