-
Mambo ya Walawi 26:5, 6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Majira yenu ya kupura nafaka yataendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu, na wakati wa kuvuna zabibu utaendelea mpaka wakati wa kupanda; nanyi mtakula mkate na kushiba na kuishi kwa usalama katika nchi yenu.+ 6 Nitaleta amani nchini,+ nanyi mtalala na hakuna yeyote atakayewaogopesha;+ nami nitawaondoa nchini wanyama wote wakali wa mwituni, na hakuna mtu yeyote atakayewashambulia kwa upanga katika nchi yenu.
-