20 Ua wa nje ulikuwa na lango lililotazama kaskazini, naye akapima urefu wake na upana wake. 21 Kulikuwa na vyumba vitatu vya walinzi kila upande. Nguzo zake za pembeni na ukumbi wake ulikuwa na vipimo sawa na lile lango la kwanza. Urefu wake ulikuwa mikono 50 na upana wake mikono 25.