-
1 Wafalme 6:31-35Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
31 Na aliitengeneza milango ya chumba cha ndani zaidi kwa mbao za msonobari, na pia nguzo za pembeni, na miimo yake, ikiwa sehemu ya tano.* 32 Alitengeneza milango hiyo miwili kwa mbao za msonobari, na kwenye milango hiyo alichonga makerubi, mitende, na maua yaliyochanua, kisha akaifunika kwa dhahabu; akawafunika makerubi hao na mitende hiyo kwa dhahabu akitumia nyundo. 33 Hivyo ndivyo alivyotengeneza miimo ya mlango wa hekalu* iliyokuwa ya mbao za msonobari, zilikuwa sehemu ya nne.* 34 Naye alitengeneza milango miwili kwa mbao za mberoshi. Mlango mmoja ulikuwa na bawaba mbili ambazo zilizunguka kwenye maegemeo, na mlango mwingine ulikuwa na bawaba mbili ambazo zilizunguka kwenye maegemeo.+ 35 Alichonga makerubi, mitende, na maua yaliyochanua, na kufunika michongo hiyo kwa bamba jembamba la dhahabu.
-